WAHITIMU WA UWAKILI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA KAZI ZA MAHAKAMA

WAHITIMU WA UWAKILI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA KAZI ZA MAHAKAMA

Like
259
0
Tuesday, 15 December 2015
Local News

WAHITIMU wa taaluma ya Uwakili Nchini wametakiwa kuzingatia sheria na kufuata utaratibu katika kufanya kazi za mahakama ili kusaidia haki kutendeka katika jamii.

Wito huo umetolewa leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George  Masaju alipozungumza katika hafla ya kuapishwa kwa Mawakili wapya zaidi ya 100 jijini Dar es salaam na kusema kuwa kitendo cha Wakili kufanya kazi bila kufuata kanuni na utaratibu wa kazi hiyo ni kosa na hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Othuman Chande amewataka Mawakili kutambua kuwa kuna chombo maalum kinachoshughulikia maadili na uadilifu wa Mawakili ambacho ni kamati ya mawakili na kwamba hadi sasa mawakili 55 tayari wamefikishwa katika chombo hicho kutokana na ukiukwaji wa maadili katika kazi.

Comments are closed.