WAHUDUMU KATIKA VITENGO VYA KUMBUKUMBU WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA TAHADHARI

WAHUDUMU KATIKA VITENGO VYA KUMBUKUMBU WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA TAHADHARI

Like
265
0
Monday, 02 May 2016
Local News

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao.

 

Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo Dkt Mohamed Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania jijini Dar es Salaam.

 

Dokta Mohamed amesema wizara hiyo, inatambua mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi wa kitengo cha kumbukumbu wanayapitia katika kazi hasa ikizingatia kuwawao ndio watu wa kwanza kukutana na wagonjwa.

Comments are closed.