WAISRAEL WALIOKUTWA NA HATIA YA MAUAJI YA MPALESTINA KUHUKUMIWA

WAISRAEL WALIOKUTWA NA HATIA YA MAUAJI YA MPALESTINA KUHUKUMIWA

Like
276
0
Monday, 30 November 2015
Slider

MAHAKAMA moja nchini Israel imewakuta waisraeli wawili na hatia ya kumuua kijana wa kipalestina mwaka wa 2014.

Washtakiwa hao wawili hawakutajwa kwa majina kwani wana umri mdogo.

Mashtaka ya mshukiwa wa tatu ambaye anatajwa kuwa ndiye aliyepanga mauaji hayo yameahirishwa ili kuruhusu uchunguzi wa kiakili.

Kijana mwenye umri wa miaka kumi na sita Mohammed Abu Khadair alichomwa moto akiwa hai mwezi julai mwaka jana baada ya kutekwa nyara Mashariki mwa Jerusalem.

Wakili wa Yosef Ben David anasema huenda anamatatizo ya kiakili

Wakili wa Yosef Ben David anasema huenda anamatatizo ya kiakili

Comments are closed.