WAJEUMANIA WAKASILIKA WACHEZAJI WAO KUPIGA PICHA NA RAIS WA UTURUKI

WAJEUMANIA WAKASILIKA WACHEZAJI WAO KUPIGA PICHA NA RAIS WA UTURUKI

Like
553
0
Wednesday, 16 May 2018
Sports
Mesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya Arsenal

Mesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya Arsenal

Nyota watatu wa Uturuki walipiga picha na bwana Erdogan (kutoka kushoto): Ilkay Gündogan (Man City); Mesut Özil (Arsenal) na Cenk Tosun (Everton)

Shirikisho la soka Ujerumani (DFB) limeshutumu wachezaji wake wa kimataifa Mesut Özil na Ilkay Gündogan kwa kupiga picha na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Wachezaji hao wawili waliozaliwa Ujerumabni, wote wenye asili ya Kituruki, walimkabidhi Erdogan fulana zao walizozisaini katika hafla moja mjini London siku ya Jumapili.

Gündogan aliandika: “kwa mtukufu rais wangu, kwa heshima kubwa.” Erdogan anafanya kampeni ya kutaka kuchaguliwa upya kama rais Uturuki.

Özil anaichezea timu ya Arsenal na Gündogan anaichezea Manchester City.

Woote wawili wanajitayarisha kwa kombe la dunia mwezi ujao nchini Urusi, ambapo Ujerumani ni miongoni mwa timu zinaozpigiwa upatu ushinda. Uturuki haikufuzu.

Wansiasa wengi Ujerumani wamewashutumu wachezaji hao wa soka, wakihoji uadilifu wao kwa maadili ya demokrasia ya Ujerumani.

Rais wa shirikisho hilo la soka Ujerumani DFB Reinhard Grindel amesema: “Soka na DFB zinalinda maadili ambayo hayaheshimiwa vya kutosha na Bwana Erdogan.

“Ndiyo sababu sio vizuri kwa wachezaji wetu wa kimataifa wakubali kuhadaiwa na kampeni yake ya uchaguzi. Kwa kufanya hivyo, wachezaji wetu hawajasaidia jitihada za DFB katika kushughulikia utangamano.”

Mkurugenzi wa DFB Oliver Bierhoff amesema: “hakuna kati yao aliyetambuwa ujumbe unaotokana na picha hiyo, lakini ni wazi kwamba ni makosa na tuazungumza nao kuhusu hilo”.

Katika ujana wake, kabla ya kuingia katika siasa katika miaka ya 90, Erdogan aliichezea timu ya Istanbul, Kasimpasa.

Erdogan, ambaye amehudumu kama kiongozi wa Uturuki kwa miaka 15 sasa anatafuta kuchaguliwa tena katika uchaguziw a dharura Juni 24.

Baada ya shutuma hizo kuzuka, Gündogan ametoa taarifa akijitetea, pamoja na wachezaji Özil na Cenk Tosun kuhusu kukutana na Erdogan.

Walikutana kando kando mwa hafla moja kwenye taasisi ya Uturuki inayowasaidia wanafunzi wa Kituruki, alieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *