WAJUMBE 5000 KUKUTANA COPENHAGEN KUHUDHURIA MKUTANO WA MASUALA YA WANAWAKE

WAJUMBE 5000 KUKUTANA COPENHAGEN KUHUDHURIA MKUTANO WA MASUALA YA WANAWAKE

Like
331
0
Monday, 16 May 2016
Global News

ZAIDI  ya wajumbe 5,000 kutoka nchi 150 wamewasili mjini Copenhagen, Denmark kuhudhuria mkutano wa wiki nzima kuhusu masuala ya wanawake.

Mkutano huo unoatajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kuandaliwa katika kipindi cha muongo mmoja kujadili masuala ya wanawake kama afya, haki na maslahi ya wanawake na wasichana umeandaliwa na shirika la kimataifa la kutetea maslahi ya wanawake la Wellbeing.

Mkutano huo unaanza leo hadi Alhamisi wiki hii na  Miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuhusu jinsi ya kupunguza vifo vya kina mama waja wazito, watoto wachanga, kukabiliana na ndoa za mapema, upangaji uzazi, ukeketaji,matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake na kupunguza maambukizi ya HIV miongoni mwa wanawake.

Comments are closed.