WAJUMBE WA BODI DAWASA WAFANYA ZIARA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU

WAJUMBE WA BODI DAWASA WAFANYA ZIARA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU

Like
353
0
Friday, 09 January 2015
Local News

Wajumbe wa kamati ya ufundi ya bodi ya maji Safi na Maji Taka Dar es salaam-DAWASA wamefanya ziara ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.

Ziara ya wajumbe hao wa kamati ya Ufundi imeanza kwa kukagua kazi ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya maji eneo la Chuo Kiukuu cha Dar es salaam, Maungio ya Mradi wa Bomba jipya yaliyopo eneo la Mpiji, ujenzi wa ofisi ya mradi wa bomba Kuu la maji kutoka Ruvu Juu Kibaha, kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha Mwendapole na upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Mladizi na Ruvu darajani

Comments are closed.