KATIKA kuhakikisha agizo la serikali la kufikisha huduma ya maji safi kwa wakazi zaidi ya milioni nne wa mkoa wa Dar es alaamu na mikoa ya jirani, mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Dar es alaamu- DAWASCO, limeanzisha zoezi maalumu kwa ajili ya kuwaunganisha wakazi hao na huduma hiyo.
Afisa uhusiano wa Dawasco EVERLASTINGI LYARO, amesema kuwa zoezi hilo limeanza rasmi tangu januari mosi mwaka huu na limegawanyika katika awamu kuu nee.
LYARO amebainisha kuwa katika awamu hizo awamu ya kwanza itaanza na wateja wote walioko kwenye maeneo ambayo yanapata maji na kunamiundo ya mabomba karibu,na kufuatiwa na maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba makubwa ya maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu yakukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.