WAKAZI DAR KUNUFAIKA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

WAKAZI DAR KUNUFAIKA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

Like
250
0
Friday, 08 January 2016
Local News

KATIKA  kuhakikisha agizo la serikali  la kufikisha huduma ya maji safi kwa wakazi zaidi ya milioni nne  wa mkoa wa Dar es alaamu na  mikoa ya jirani,  mamlaka ya maji safi na maji taka  mkoa wa Dar es alaamu- DAWASCO,  limeanzisha zoezi maalumu kwa ajili ya kuwaunganisha wakazi hao na  huduma hiyo.

 

Afisa uhusiano wa Dawasco  EVERLASTINGI  LYARO,  amesema kuwa zoezi hilo limeanza rasmi tangu januari mosi mwaka huu na limegawanyika katika awamu kuu nee.

 

LYARO amebainisha kuwa katika awamu hizo awamu ya kwanza itaanza na wateja wote walioko kwenye maeneo ambayo yanapata maji na kunamiundo ya mabomba karibu,na kufuatiwa na maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba makubwa ya maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu yakukosekana  kwa miundo mbinu ya usambazaji.

Comments are closed.