WAKAZI DAR WAANZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

WAKAZI DAR WAANZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Like
267
0
Wednesday, 22 July 2015
Local News

WAKAZI wa Mkoa wa Dar es salaam leo wameanza Zoezi la kujiandikisha katika Dafutari la Kudumu la mpiga kura kwa njia ya Kielektroniki- BVR.

Efm imepita katika vituo mbalimbali vya kujiandikishia na kushuhudia misururu ya watu ambao wamewahi vituoni humo kwa lengo la kutimiza haki yao hiyo ya msingi kikatiba.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wamedai kuchelewa kwa waandikishaji katika vituo, ikizingatiwa kuwa ni siku za kazi hivyo kuiomba Tume ya Uchaguzi kulizingatia hilo ili watu wapate nafasi ya kujiandikisha na kuwahi katika shughuli zao.

Comments are closed.