WAKAZI DAR WAOMBA KUTAZAMWA UPYA VIWANGO VYA NAULI

WAKAZI DAR WAOMBA KUTAZAMWA UPYA VIWANGO VYA NAULI

Like
253
0
Thursday, 08 October 2015
Local News

WAKAZI  wa jiji la Dar es salaam wamewaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri kuangalia upya viwango vya bei ya nauli  mara baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA kushusha bei ya mafuta .

Wakizungumza na E fm baadhi ya wakazi hao  wamewaomba  wamiliki kuwapunguzia bei za  nauli  kwani bei za mafuta zimeshuka kutoka bei za awali ambapo zilikuwa shilingi 2300 kwa lita moja ya petroli  tofauti na ilivyo sasa ambapo bei ya petrol kwa lita moja ni shilingi 2000 na senti 86.

Naye mmoja wa watendaji wa chama cha wamiliki wa mabasi nchini-TABOA, Mbazi Mbazi amesema kuwa mchakato wa ushukaji wa nauli unategemea mambo mengi hivyo kushuka kwa  mafuta siyo kigezo pekee kinachochangia kushuka kwa nauli.

Comments are closed.