WAKAZI na wafanyabiashara wa eneo la banana jijini Dar es Salaam wameiomba halmashauri ya manispaa ya Ilala kuondoa dampo la taka ambalo siyo rasmi ambazo zinatupwa kandokando ya barabara ili kuweza kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Takataka hizo ambazo zimewekwa katika eneo ambalo siyo rasmi zimekaa kwa muda mrefu bila kuondolewa hali inayosababisha eneo hilo kuwa na harufu mbaya kwa wakazi hao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na baadhi ya wakazi na wafanyabiashara ambao wanafanya shughuli zao karibu na eneo hilo.