WAKAZI WA BANANA WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

WAKAZI WA BANANA WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

Like
320
0
Monday, 15 December 2014
Local News

WAKAZI  na  wafanyabiashara  wa  eneo  la banana  jijini Dar es Salaam  wameiomba halmashauri ya  manispaa  ya Ilala  kuondoa  dampo  la taka  ambalo  siyo rasmi ambazo  zinatupwa  kandokando  ya  barabara ili  kuweza kuzuia  magonjwa  ya  mlipuko.

Takataka  hizo  ambazo  zimewekwa  katika  eneo  ambalo siyo rasmi  zimekaa  kwa  muda  mrefu bila  kuondolewa  hali  inayosababisha eneo  hilo  kuwa  na harufu  mbaya  kwa  wakazi  hao.

Hayo  yamesemwa  leo  jijini Dar es Salaam  na  baadhi  ya wakazi  na  wafanyabiashara  ambao wanafanya  shughuli  zao  karibu na  eneo hilo.

 

Comments are closed.