WAKAZI WA JANGWANI WAMEIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA MIUNDOMBINU

WAKAZI WA JANGWANI WAMEIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA MIUNDOMBINU

Like
309
0
Tuesday, 22 September 2015
Local News

WANANCHI wa mtaa wa mtambani B kata ya jangwani Jijini Dar es salaam wameitaka serikali kuangalia upya miundombinu ya mabomba yaliyowekwa kwa ajili ya kutoa maji ya mvua kwenye nyumba za gorofa ambayo hutumika kutoa maji hata kipindi cha kiangazi.

Wakizungumza na kituo hiki wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa hali hiyo imekithiri huku wakazi wa nyumba hizo wakionesha kutojali hali ya mazingira ya wale wanaofanya shughuri mbalimbali chini ya gorofa hizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mtambani B Gungu Tambaza amesesema kuwa hali hiyo imetokana na wataalamu wa Afya katika kata kutokuwa wafuatiliaji wa masuala ya usafi wa mazingira.

Comments are closed.