WAKAZI WA KIMARA Baruti Jijini Dar es salaam wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya Mripuko baada ya eneo wanalohifadhia taka kujaa.
Wakizungumza na EFM wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikuwa wakiweka taka hizo katika magari ya kuzolea taka lakini cha kushangaza magari hayo hayapiti hali inayowapelekea kukaa na taka hizo majumbani huku wengine wakizipeleka eneo la kilungule kwa ajili ya kutupa.
Wameeleza kuwa tarari wameshatoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ili kutatua tatizo hilo lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuweza kumaliza tatizo hilo.