WAKAZI WA KIRUMBA, MWANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA UWEKAJI ALAMA

WAKAZI WA KIRUMBA, MWANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA UWEKAJI ALAMA

Like
434
0
Thursday, 10 December 2015
Local News

WAKAZI wa mtaa wa Ibanda kata ya kirumba  Jijini Mwanza wanatarajiwa kupokea  mradi wa  uwekaji Alama katika maeneo yao ili kupunguza migogoro ya Ardhi iliyokithiri katika kata yao.

Hayo yamekuja mara baada ya  mtaa huo kuwa na migogoro ya ardhi ya mara kwa mara  na kuwaathiri wananchi waishio katika maeneo hayo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Ephrahim Nkingwa amesema tayari amewasilisha barua kwa mkurugenzi wa Jiji ya kuomba upimaji shirikishi ili kuhakikisha maeneo yote ya mtaa huo yanapimwa na kuepusha migogoro hiyo.

 

Comments are closed.