WAKAZI WA MABONDENI DAR WATAKIWA KUHAMA

WAKAZI WA MABONDENI DAR WATAKIWA KUHAMA

Like
215
0
Monday, 30 March 2015
Local News

KUFATIA Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam baadhi ya Wananchi wamewataka watu waishio maeneo ya mabondeni, kuhama maeneo hayo ili kunusuru Maisha, Mali  pamoja na kuepusha gharama kwa Serikali pindi maafa yanapotokea.

Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Jiji la Dar es salaam, bado lina maeneo mengi yaliyosalama, hivyo wanapaswa kuepuka utamaduni wa kwamba maisha bora yanapatikana katikati ya Mji bila kujali Usalama wa maeneo hayo.

Wananchi hao wamesema imekuwa ni Desturi ya Watanzania kulaumu Serikali pindi maafa yanapotokea, wakati Serikali imekuwa ikitoa tahadhari mara kwa mara kwa watu hao kuhama maeneo ya Mabondeni.

Comments are closed.