WAKAZI WA NGARENARO WAMO HATARINI KUPATA MAGONJWA

WAKAZI WA NGARENARO WAMO HATARINI KUPATA MAGONJWA

Like
251
0
Monday, 24 November 2014
Local News

utupaji watoto Wachanga umekithiri katika mto Ngarenaro jijini Arusha hali inayohatarisha magonjwa kwa watumiaji wa Maji yanayotoka katika Mto huo.

Kutokana na hali hiyo wakazi waliopo karibu na mto huo wamelazimika kufanya usafi wa mazingira mara kwa mara.

Mkazi wa eneo la Kambi ya Fisi ambako pia mto huo unapita MWAJUMA MBAGA amesema wanalazimika kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzake katika kuulinda mto huo.

Kazi ya kuusafisha mto huo inafanywa na wakazi wa eneo hilo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Arusha na kikundi cha Mazingira cha Nitoke Vipi

Comments are closed.