ITALIA imefanikiwa kuokoa Wakimbizi Elfu-2 waliokuwa wakisafiri kwa boti kutoka Libya kuelekea Ulaya.
Wakimbizi hao walikuwa kwenye Meli ya Jeshi na boti za Shirika la Uokozi Baharini na pia kwenye boti za Polisi wa Mpakani.
Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi ya Italia imeeleza kuwa baadhi ya waokozi wametishiwa na wanaume waliokuwa wamebeba Silaha na ambao wanaaminika kuwa ndio waliowasafirisha Wakimbizi hao.