WAKIMBIZI 500 WAHOFIWA KUFA KWENYE BAHARI YA MEDITERANIA

WAKIMBIZI 500 WAHOFIWA KUFA KWENYE BAHARI YA MEDITERANIA

Like
380
0
Thursday, 21 April 2016
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia wakimbizi limehofu kuwa huenda wakimbizi 500 wamefariki kwenye bahari ya Mediterania walipokuwa njiani kuelekea Italia.

Hata hivyo msemaji wa shirika hilo amewaambia waandishi wa habari kwamba haijulikani ni lini wakimbizi hao wamefariki lakini amesema wachunguzi wanawahoji wakimbizi 41 walionusurika.

Umoja wa Mataifa umebaisha kwamba miongoni mwa watu waliookolewa walikuwa wakimbizi kutoka Somalia, Ethiopia, Misri na Sudan.

Comments are closed.