WAKUFUNZI WA VYUO VYA UALIMU NCHINI WATAKIWA KUKUZA VIWANGO VYA UMAHIRI VYA TEHAMA

WAKUFUNZI WA VYUO VYA UALIMU NCHINI WATAKIWA KUKUZA VIWANGO VYA UMAHIRI VYA TEHAMA

Like
419
0
Friday, 24 July 2015
Local News

KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.

 

Ametoa kauli hiyo mjini Bagamoyo wakati akifungua  kongamano linalohusu upitiaji waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

 

Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin  Kulwa amesema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.

TEHAMA3 TEHAMA4 TEHAMA

Comments are closed.