WAKUU WA IDARA WA MANISPAA ZA JIJI LA DARESALAAM WALA KIAPO KUTAFUTA WATUMISHI HEWA

WAKUU WA IDARA WA MANISPAA ZA JIJI LA DARESALAAM WALA KIAPO KUTAFUTA WATUMISHI HEWA

Like
407
0
Monday, 02 May 2016
Local News

WAKUU wa Idara zote za Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wanatoa majina yote ya watumishi hewa ndani ya muda wa siku saba kuanzia leo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali nchini, maafisa utumishi, wakurugenzi wa wilaya na viongozi wengine.
Baada ya kutoa agizo hilo Mheshimiwa makonda amewataka Wakuu wa idara zote za mkoa huo, kusaini Mkataba wa kiapo cha kutojihusisha na suala la kuwaficha watumishi hewa na endapo mkuu wa idara yoyote atathibitika kuwa na mtumishi hewa kwenye idara yake kuanzia wiki ijayo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Comments are closed.