WALIOFARIKI MKASA WA JENGO NAIROBI WAONGEZEKA

WALIOFARIKI MKASA WA JENGO NAIROBI WAONGEZEKA

Like
301
0
Wednesday, 04 May 2016
Global News

IDADI ya watu waliofariki baada ya jumba la ghorofa sita kuporomoka siku ya Ijumaa imeongezeka baada ya miili zaidi kupatikana kwenye vifusi.

Maafisa wa uokoaji wamepata miili mitatu zaidi na kufikisha miili 26, ambayo ni idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha.

Hata hivyo Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limeeleza kuwa Watu 93 bado hawajulikani walipo.

Comments are closed.