WALIOJARIBU KUSHAMBULIA NDEGE WAHUKUMIWA MAISHA JELA

WALIOJARIBU KUSHAMBULIA NDEGE WAHUKUMIWA MAISHA JELA

Like
266
0
Monday, 30 May 2016
Local News

Mahakama ya kijeshi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imewahukumu kifungo cha maisha wanaume wawili ambao walipatikana na hatia ya kupanga shambulizi dhidi ya ndege ya shirika la Daallo mwezi Februari.

Bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu ikiwa safarini kwenda nchini Djibouti.
Shimo lilitobolewa kando mwa ndege hiyo lakini hata hivyo ndege haikusambaratika.

Abiria mmoja ambaye alitupwa nje ya ndege hiyo aliaga dunia na wengine wawili wakajeruhiwa.
Washtakiwa wengine wanane walihukumiwa vifungo vya kati ya miezi sita na miaka minne.
Hao ni pamoja na waliokuwa wafanyikazi wa uwanja wa ndege na maafisa wa ulinzi.

Comments are closed.