WAMILIKI WA MAGARI WAMETAKIWA KUYAKATIA BIMA MAGARI YAO

WAMILIKI WA MAGARI WAMETAKIWA KUYAKATIA BIMA MAGARI YAO

Like
351
0
Wednesday, 08 June 2016
Local News

WAMILIKI na Madereva wa Magari nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa magari yote yanayotembea barabarani yamekatiwa bima iliyotolewa na kampuni iliyosajiliwa na mamlaka ya bima  kufuatia badala ya kutumia bima feki.

Akizungumza na E fm jijini Dar es salaam leo , Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania- TIRA, Paul Ngwembe amesema kuwa sheria ya bima ya mwaka 2009 inayosimamia masuala ya bima inataka kila gari linalotembea barabarani liwe na bima lakini kumekuwepo na baadhi ya wamiliki au madereva ambao sio waaminifu wanaotembeza magari yao bila kuwa na bima au ya kiwa na bima feki jambo ambalo ni kinyume na sheria kanuni na taratibu za barabarani na husabisha usumbufu mkubwa endapo ajali itatokea.

 

Comments are closed.