WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI WALAANI MUSWADA MPYA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI WALAANI MUSWADA MPYA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

Like
204
0
Tuesday, 26 May 2015
Local News

WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini-MOAT na waandishi wahabri wamelaani muswada mpya wa sheria ya vyombo vya habari uliotaka kuwasilishwa katika kikao cha bunge kilichopita kwa hati ya dharula kwa kuwa baadhi ya vipengele kwenye muswaada huo unapunguza uhuru wa vyombo vya habari.

Hata hivyo muswaada huo wenye kasoro nyingi unaonesha kuwa kuna hila chafu za kutaka kupitisha sheria hiyo bila kuhusisha wadau wa tasnia hiyo ili kudhibiti vyombo binafsi na wananchi wasiweze kutoa na kupata taarifa jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa MOAT Dokta REGNALD MENGI amesema vyombo vya habari vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa kwa mwanadamu yeyote.

Comments are closed.