WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI

WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI

Like
226
0
Monday, 20 July 2015
Local News

WAMILIKI wa vyombo vya moto hususani madereva wametakiwa kutii sheria bila shuruti kwa kufuata utaratibu wa usalama ili kuepusha madhara yanayojitokeza mara kwa mara barabarani.

 

Rai hiyo imetolewa na Askari wa usalama barabarani eneo la Kawe WIPI HAPPY wakati akizungumza na kituo hiki leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na mmoja wa madereva ambaye hakutaka kutii sheria iliyowekwa na Askari huyo.

 

Hali hiyo imekuja kufuatia Lori la mizigo kufunga barabara ya Mwai Kibaki kutokana na kushindwa kugeuka katika sehemu hiyo ya barabara hali iliyosababisha foleni kubwa ya magari na hivyo Askari kuweka utaratibu wa magari kupita eneo hilo kwa zamu.

 

Comments are closed.