MAWAZIRI wa Mambo ya Ndani kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels katika mkutano wa dharura kujadili hali ya wakimbizi.
Watajadili mapendekezo ya kuwapa makazi wakimbizi 120,000 katika sehemu mbalimbali za umoja huo waliowasili nchini Ugiriki, Italia na Hungary.
Mawaziri hao watajadili pia kuanzishwa kwa vituo maalumu kuwasaidia, kuwasajili na kuwachunguza wakimbizi wanaowasili katika mataifa hayo matatu ya eneo la Schengen.