WANADIPLOMASIA KUKUTANA VIENNA LEO KUIJADILI SYRIA

WANADIPLOMASIA KUKUTANA VIENNA LEO KUIJADILI SYRIA

Like
291
0
Thursday, 29 October 2015
Global News

WANADIPLOMASIA wa ngazi za juu duniani wanakutana mjini Vienna leo kujaribu kusaka ufumbuzi wa pamoja wa namna ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Wanadiplomasia hao kutoka Urusi, Marekani, Saud Arabia na Uturuki wanakutana kwa duru ya pili ya mazungumzo kuhusu Syria, baada ya ile ya wiki iliyopita kabla ya kuitishwa mkutano utakaowajumuisha wanadiplomasia wa eneo hilo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif atajiunga na wenzake kutoka Uingereza, Misri, Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya katika wakati ambapo jumuia ya kimataifa inatafuta njia ya kumaliza miaka minne ya umwagaji damu nchini Syria.

Comments are closed.