WANAFUNZI VYUONI WATAKIWA KUJIHESHIMU NA KUJITHAMINI

WANAFUNZI VYUONI WATAKIWA KUJIHESHIMU NA KUJITHAMINI

Like
306
0
Wednesday, 28 January 2015
Local News

WITO umetolewa kwa wananfunzi wa vyuo mbalimbali nchini kujenga tabia ya kujiheshimu na kujitathimini ikiwa ni pamoja na kufuata kile kilichowapeleka chuoni ili kuweza kulinda heshima na utu wa mwanamke

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na aliyekuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM na mwanaharakati wa kutetea haki za kijinsia HILDA KIWASILI ambapo amesema kuwa wanafunzi wengi hasa wa vyuo vikuu wamekuwa na tabia ya kujiingiza katika makundi ya tamaa na kusahau kinachowapeleka vyuoni jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

Aidha amebainisha kuwa wanachuo wengi wamekuwa na tabia za kutamani mambo makubwa yanayozidi uwezo wao hali inayopelekea kuishi maisha ya tamaa na anasa ili kukidhi mahitaji yao huku wakijiingiza katika mambo ya hatari.

Comments are closed.