WANAHARAKATI WACHINJWA DERNA

WANAHARAKATI WACHINJWA DERNA

Like
281
0
Wednesday, 12 November 2014
Global News

WANAHARAKATI watatu wa kisiasa nchini Libya wameuawa kwa kuchinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam. Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi.

Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu.

Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la IS.

Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.

Comments are closed.