WANAJESHI 5 WAPEWA MAFUNZO YA KIVITA YA MAJINI KUPAMBANA NA MAHARAMIA UKANDA WA BAHARI YA HINDI

WANAJESHI 5 WAPEWA MAFUNZO YA KIVITA YA MAJINI KUPAMBANA NA MAHARAMIA UKANDA WA BAHARI YA HINDI

Like
391
0
Monday, 24 November 2014
Local News

WANAJESHI kumi na tano wa Jeshi la Wananchi la Tanzania leo wamepewa mafunzo ya kivita ya majini ya namna ya kupambana na Maharamia kwenye Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Balozi wa Italia Dokta LUIGI SCOTTO amebainisha kuwa wanajeshi hao watafundishwa namna ya kutega na kutegua zana za kivita yakiwemo mabomu yanayotumiwa na maharamia kwenye shughuli za utekaji nyara wa Meli za mizigo na abiria.

Dokta LUIGI ameeleza kuwa katika harakati za kupambana na maharamia hao wameimarisha ulinzi kwa kujenga Ngome ya Meli za kivita maeneo ya ukanda wa pwani nchini Somalia kwani ndiyo sehemu kuu ya maficho ya maharamia.

Amebainisha kuwa Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Umoja wa Ulaya imesaini mkataba wa kudhibiti vitendo vya kiharamia kwenye ukanda wa bahari ya hindi April mwaka huu.

Comments are closed.