Wanajeshi Gabon wajaribu kupindua serikali ya Ali Bongo ambaye yuko Morocco

Wanajeshi Gabon wajaribu kupindua serikali ya Ali Bongo ambaye yuko Morocco

Like
756
0
Monday, 07 January 2019
Global News

Kundi la wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville. Shirika la habari la AFP inasema milio ya risasi imesikika jijini humo.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa.

Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

Wanajeshi hao wametangaza kwamba wanataka kuunda ‘Baraza la Ufufuzi/Ukombozi’.

Wamekosoa hotuba ya Mwaka Mpya iliyotolewa na Rais Bongo mnamo 31 Desemba, na wanasema kwenye hotuba hiyo mawazo yake yalionekana kutotiririka na sauti yake ilikuwa dhaifu.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *