Moto mkubwa waunguza msitu na kuua watu 20 Ugiriki

Moto mkubwa waunguza msitu na kuua watu 20 Ugiriki

Like
627
0
Tuesday, 24 July 2018
Global News

Penteli, Athens, Greece Julai 23, 2018

Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 20, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo.

Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto,wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo,huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens.

Kikosi cha uokoaji kinaendelea na jitihada za kuwapata watalii 10 ambao walitoweka katika harakati za kujiokoa na moto huo.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema watafanya lolote linalowezekana kibinadamu kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu.

Neo Voutsa, kaskazini mashariki mwa Athens, Ugiriki, 23 Julai 2018.

Hata hivyo waziri huyo amelazimika kukatisha ziara yake ya Bosnia ili kusaidia uratibu wa hali hiyo,ambayo vikozi vya uokoaji vinasema ni mbaya kuwahi kutokea.

Msemaji wa serikali Dimitris Tzanakopoulos amethibisha kuwa watu 20 wamekufa kutokana na moto huo, amefafanua kuwa wale waliokwama upande wa baharini takribani kilomita 40 kaskazini mashariki mwa mji wa Athens ndiyo waliokufa wakiwa nyumbani kwao na wengine kwenye magari.

Watu 104 wamejeruhiwa kati yao 11 wakiwa katika hali mbaya, lakini watoto 16 nao wamejeruhiwa.

Waziri mkuu Tsipras amesema hali ya hatari imetangazwa katika Attica karibu na mji wa Athens.

Moto Kineta, karibu na Athens, Julai 23, 2018

Nchi za Italia, Ujerumani, Poland na Ufaransa wametuma misaada ya ndege, magari na watalaamu wazima moto.

Huu ndio moto mbaya zaidi wa nyikani kukumba Ugiriki tangu mwaka 2007 pale watu kadha walippouawa na moto rasi ya Peloponnese kusini mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *