WANAJESHI WANAMAJI WANNE WAUAWA MAREKANI

WANAJESHI WANAMAJI WANNE WAUAWA MAREKANI

Like
191
0
Friday, 17 July 2015
Global News

MTU mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamaji wa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja  na Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani.

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

Kufuatia tukio hilo maeneo kadhaa yamefungwa zikiwamo hospitali na shule ili kuchukua tahadhari.

 

Comments are closed.