WANAJESHI WATANO WAUAWA KUTOKANA NA MAPIGANO UKRAINE

WANAJESHI WATANO WAUAWA KUTOKANA NA MAPIGANO UKRAINE

Like
245
0
Thursday, 04 June 2015
Global News

WANAJESHI watano wa Ukraine wameuawa katika mapigano karibu na  mji unaoshikiliwa na serikali wa Maryinka, ambako waasi wanaoipendelea Urusi wakijaribu kusonga mbele.

Msemaji wa Ikulu mjini Kiev Yuri Biryukov, amesema kuwa katika ukurasa wake wa Faceboock, kwamba  raia 39 wa Ukraine wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema kwamba  waasi wanaotaka kujitenga, wakitumia vifaru  na mizinga walijaribu kuviteka vituo vya serikali karibu na Maryinka, mashariki mwa mji unaoshikiliwa na waasi wa Donetsk, ikiwa ni kinyume na usitishaji mapigano uliotangazwa mwezi Februari.

Hata hivyo taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa waasi hao wamerudishwa nyuma na majeshi ya serikali.

Comments are closed.