WANAJESHI WAZIDI KUTEKETEA AFGHANSTAN

WANAJESHI WAZIDI KUTEKETEA AFGHANSTAN

Like
358
0
Friday, 07 November 2014
Global News

KATIBU MKUU wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg, amesema idadi ya wanajeshi wa Afghanistan wanaokufa imeongezeka zaidi kwa sababu ya kuchukuwa kwao dhima ya juu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Taliban.

Takwimu zilizotolewa wiki hii zinaonesha kuwa hadi kufikia sasa, wanajeshi wa Kiafghani waliouawa mwaka huu pekee ni 4,634.

Stoltenberg ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza nchini Afghanistan tangu achukue wadhifa huo mwanzoni mwa mwezi Oktoba, alikutana na Rais Ashraf Ghani hapo jana na leo anaelekea kwenye mji wa mashariki wa Herat, kuwakumbuka wanajeshi wa NATO 53 wa Italia waliopoteza maisha huko.

Comments are closed.