WANANCHI DAR KUTOWAFUMBIA MACHO VIONGOZI WALAGHAI

WANANCHI DAR KUTOWAFUMBIA MACHO VIONGOZI WALAGHAI

Like
266
0
Friday, 28 August 2015
Local News

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam wamesema hivi sasa wanahitaji mabadiliko kutoka kwa viongozi wanaotarajia kuingia madarakani ili jamii iweze kuwaamini.

Wakizungumza na EFM katika nyakati tofauti wananchi hao wamesema hawatawafumbia macho viongozi wanaodiriki kuwalaghai wananchi kwa  kuwapa fedha na vitu mbalimbali kwa lengo la kuwachagua na kuwaomba watu wote kuwa makini na kumpata kiongozi bora na mwadilifu.

Aidha wamesema hali ngumu ya maisha ndio inayopelekea wananchi kujiingiza katika  kupokea pesa na vitu mbalimbali vya ushawishi ili waweze kujikimu kimaisha pasipo kujua madhara yake baadae.

Comments are closed.