WANANCHI wa wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 1.8 kwa siku.
Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania dokta Mohammed Akbar amesema wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini jambo ambalo limeonesha mafanikio makubwa.
Dokta Akbar amesema endapo maji hayo yataunganishwa kwenye miundombinu iliyopo katika mji huo yatakidhi mahitaji ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki Sita na Elfu mbili kwa siku.