WANANCHI PWANI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

WANANCHI PWANI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Like
305
0
Tuesday, 07 July 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imetoa wito kwa wananchi wote wa Mikoa ya Pwani  kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wapate haki yao ya kupiga Kura na kuchagua Viongozi bora katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imeeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo kwa mkoa wa Pwani unaanza leo hadi julai 20 mwaka huu kabla ya kuanza mkoa wa Dar es salaam.

Mbali na kutoa ratiba ya uboreshaji wa daftara la kudumu la wapiga kura kwa mkoa huo pia wananchi wameshauriwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha Zoezi hilo linafikia malengo yaliyowekwa.

Comments are closed.