WANANCHI WA JIMBO LA MTAMA MKOANI LINDI WAMTIKISA MEMBE

WANANCHI WA JIMBO LA MTAMA MKOANI LINDI WAMTIKISA MEMBE

Like
382
0
Thursday, 12 February 2015
Local News

WANANCHI wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemtaka mbunge wa jimbo hilo Bernald Membe anayemaliza muda wake kutokujishughulisha kwa namna yoyote kuwatafutia mrithi wa nafasi ya ubunge kwani kwa kufanya hivyo hawata mchagua.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wamesema kitendo chochote cha kupingana na chaguo la wananchi kitasababisha Jimbo la Mtama kuwa na wakati mgumu na kwamba wanahitaji mbunge mwenye uchungu na jimbo kwa kuwa jimbo hilo lipo nyuma kwa Nyanja zote za Kielimu, Afya na Miundombinu.

Mwenyekiti wa wanaharakati hao kutoka Mtama Bwana ISSA MBENDE amesema wanahitaji viongozi wenye uchungu na jimbo hilo, badala ya kuletewa kiongozi mwenye kuangalia maslahi yake binafsi kulingana na utashi wa kiongozi aliyemleta.

Comments are closed.