WANANCHI WA TUNISIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU LEO

WANANCHI WA TUNISIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU LEO

Like
345
0
Monday, 24 November 2014
Global News

WANANCHI wa Tunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu kutokea vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011.

Mapinduzi hayo yalisababisha vuguvugu hilo la mabadiliko katika nchi nyingine za Kiarabu.

Miongoni mwa wagombea katika kinyang’anyoro hicho ni mwanasiasa mkongwe Beji Essabsi, aliyewahi kushika nafasi muhimu wakati wa utawala kabla ya kutokea mapinduzi.

Bwana Beji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo ameahidi kurejesha kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.

 

Comments are closed.