WANANCHI WAIPONGEZA CCM KWA KUPATA MGOMBEA WAKE

WANANCHI WAIPONGEZA CCM KWA KUPATA MGOMBEA WAKE

Like
224
0
Monday, 13 July 2015
Local News

BAADHI ya Wananchi wamekipongeza Chama cha Mapinduzi -CCM- kwa Kumpitisha Dokta John Magufuli kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Tano kwa tiketi ya chama hicho.

Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Chama hicho  kimewapatia Watanzania aina ya Mtu ambae wamekua wakimhitaji kwa kipindi kirefu kwani Watanzania wanahitaji mtu mwenye ujasiri mkubwa wa kutoa maamuzi kama alivyo Dokta Magufuli kwani mara nyingi amekua akichukua maamuzi magumu katika utendaji wake akiwa katika wizara mbali mbali alizowahi kupita.

Wananchi hao wamemtaka Mheshimiwa Magufuli kuendelea na Msimamo alionao katika Utendaji wake wa kazi.

Comments are closed.