KUFUATIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC– kutangaza kuongeza siku nne za kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura kwa wakazi wa Dar es salaam kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi ulioonekana katika vituo mbalimbali vya uandikishaji, baadhi ya wakazi wa mkoa huo wameipongeza hatua hiyo.
Wakizungumza na Efm leo katika vituo mbalimbali vya kujiandikisha katika Daftari hilo la kudumu la mpiga kura kwa njia ya kielektroniki,-BVR, wakazi hao wamesema uamzi huo ni wabusara nakuwataka wananchi kuitumia nafasi hiyo vizuri badala ya kusubiri kulalamika kuwa hawakutendewa haki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu DAMIAN LUBUVA alisema kuwa takwimu zinaonesha hadi kufikia jana jumla ya wananchi milioni 18, laki nane na ishirini na sita mia saba kumi na nane wameshaandikishwa katika Daftari hilo.