WANANCHI WAIUNGA MKONO SERIKALI KUTUMBUA MAJIPU

WANANCHI WAIUNGA MKONO SERIKALI KUTUMBUA MAJIPU

Like
268
0
Monday, 22 February 2016
Local News

WAKATI Serikali kupitia Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ikiendelea na mpango wa kufukuza wafanyakazi wasiokidhi viwango vya utendaji kazi kwa kutumia Kauli ya Kutumbua Majipu iliyoanzishwa na Rais wa Awamu ya Tano Dokta John Pombe Magofuli, Wananchi wengi wameonesha kuunga mkono hatua hiyo.

Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa mazoea na kufanya Ofisi na Taasisi za Serikali kama mali zao hivyo kitendo cha kuwaondosha kitasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.

EFM imepata nafasi ya Kuzungumza na Mtaalamu wa elimu ya tabia za binadamu-Anthropologist-Kutoka Chuo kikuu cha Havad tawi lililopo Nchini Israel Dokta Joseph Terry ambaye amebainisha kuwa fukuzafukuza hiyo itasaidia kuleta ufanisi katika utendaji kazi.

Comments are closed.