WANANCHI WALIA NA DAWASCO KUKOSEKANA KWA MAJI KINONDONI

WANANCHI WALIA NA DAWASCO KUKOSEKANA KWA MAJI KINONDONI

Like
367
0
Tuesday, 18 August 2015
Local News

BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa Mkunguni A Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia Mamlaka ya maji safi na maji taka-Dawasco kwa kutokuwa na huduma ya maji kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Wakizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam wananchi hao wamesema kuwa tatizo la kukosa maji eneo lao lipo kwa muda mrefu ingawa bado hawajui sababu japokuwa mabomba ya maji yapo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco Evertasting Lyaro ameeleza kuwa tatizo hilo si la dawasco isipokuwa limechangiwa na miundombinu ya ujenzi wa barabara na kuchangia kukosekana kwa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo.

Comments are closed.