WANANCHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA USAFI KWENYE MAADHIMISHO YA UHURU

WANANCHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA USAFI KWENYE MAADHIMISHO YA UHURU

Like
248
0
Monday, 07 December 2015
Local News

WANANCHI wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono Juhudi za Serikali za kufanya usafi siku ya Maadhimisho ya Uhuru Disemba 9 mwaka huu ili kuweka mazingira safi na kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Kituo cha Radio cha 93.7 Efm Denis Ssebo wakati akizungumza na waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa zoezi hilo kwa kila mtu ambapo amesema Efm radio kwa kushirikiana na  Benki ya DTB, Wasanii wa Bongo movie na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa pamoja  watafanya usafi kwenye barabara inayoanzia Moroco kuelekea Magomeni.

 

 

Comments are closed.