WANANCHI WAMETAKIWA KUTII SHERIA ZA NCHI NA TUME YA UCHAGUZI

WANANCHI WAMETAKIWA KUTII SHERIA ZA NCHI NA TUME YA UCHAGUZI

Like
224
0
Wednesday, 21 October 2015
Local News

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi MATHIAS CHIKAWE  amewataka  wananchi kutii sheria za nchi na zile za tume ya uchaguzi zinazoongoza uchaguzi mkuu sambamba na kufuata maelekezo yatakayotolewa na tume kabla na baada ya kupiga kura kwani kila mtanzania ana wajibu wa kuilinda amani kwa kufuata sheria za nchi bila kushurutishwa.

 

Akizungumza na Efm Radio,  leo jijini dar es salaam, waziri CHIKAWE amesema kuwa watanzania watambue baada ya uchaguzi mkuu maisha yanapaswa kuendelea kama kawaida hivyo itikadi za vyama vya siasa zisiwatofautishe na kuwajengea chuki,uhasama au uadui kwani wote ni wamoja na wanatakiwa kuishi kwa amani  na ushirikiano katika kuendeleza taifa.

Comments are closed.