WANANCHI WANUFAIKA NA MRADI WA MASHINE YA KUKAMULIA ALIZETI BABATI

WANANCHI WANUFAIKA NA MRADI WA MASHINE YA KUKAMULIA ALIZETI BABATI

Like
376
0
Wednesday, 16 September 2015
Local News

WANANCHI wa Kijiji cha Endanoga Wilayani Babati Mkoani Manyara, imeelezwa kuwa wamenufaika na mradi wa mashine ya kukamulia alizeti wenye thamani ya shilingi  milioni 205  uliodhaminiwa  kwa ushirikiano wa  Serikali na wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela ameitaka jamii ya eneo hilo kuutunza mradi huo uliofadhiliwa na Wizara ya kilimo, chakula na ushirika iliyotoa shilingi milioni 197.9, Halmashauri ya mji shilingi milioni 3.2  na jamii shilingi milioni 7.9.

Meela amesema mashine hiyo itatumika kuongeza uchumi wa jamii inayozunguka eneo hilo kwani watakuwa wanaongeza thamani ya mazao yao na kupata faida kubwa tofauti na awali walipokuwa wanauza alizeti zikiwa ghafi.

Comments are closed.