WATANZANIA hususani wakazi wa Jiji la Dar es salaam wameombwa kuwa makini katika matumizi ya vyakula na mazingira wanayo ishi kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshasababisha vifo kwa watu watatu.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kuenea kwa ugonjwa huohatari.
Naye mganga Mkuu wa wilaya hiyo dokta Azizi Msuya amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema hasa wanapohisi uwepo wa dalili za Kipindupindu ikiwemo kutapika, kuripoti kwenye kituo cha afya ili kuweza kupata huduma mapema.