WANANCHI wametakiwa kujitokeza na kujiunga na mifuko ya jamii ya uwekezaji wa pamoja ya UTT AMIS ili kunufaika na faida mbalimbali za uwekezaji zinazotokana na kuongezeka kwa thamani ya vipande kufuatia kukua kwa mifuko hiyo ya uwekezaji kwa asilimia 25 kutoka bilioni 179 na kufikia bilioni 227 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita .
Akisoma ripoti ya mifuko hiyo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Afisa mwendeshaji mkuu wa UTT AMIS Simon Migangala amesema hayo ni mafanikio makubwa katika mifuko hiyo kwakuwa idadi ya wawekezaji katika mifuko imekuwa .